Nov 11, 2006

Tanzania na education yetu= Mchezo wa kuigiza!
Jamaa mmoja Karl Marx huyu huyu unayemjua, ambaye sisi wa Education tunamstudy kwenye Sociology, anasema endapo mtu anataka kujua the position of the teacher in any society one must look at
  • the value his/her society places in education
  • the organization of the education system of that society
  • the training required for a teacher
    and;
  • the kinds of pipo likely to be attracted to his/her occupation
Sasa my problem is not that teachers are not respected in Bongoland!
Hebu fikiria hii, ili mtu ateach primary school lazima awe na grade III A, GOOD! Lakini huyu mtu ndiye yule yule aliye fail form four. Nina maana kwamba ukipata div. two mbaya au three form four, you qualify to go to teaching college vivyo hivyo kwa A-level ukifelifeli basi utaenda kuchukua education. Tatizo ni kwamba hii negative notion imekuwapo toka longtaim hadi inafikia mahali mtu ukisema unasoma education unaangaliwa kana kwamba umedunda f.4.
We should agree that if we really want to prepare a nation of trained, educated individuals lazima tutakuwa careful kuhakikisha our pipo are given the best education the state can offer using the best teachers possible. Ni aibu kurecruit walimu kutoka Kenya kuja kufundisha curriculum ya Tanzania.

KUPIGIKA!!!
Hii niliishuhudia majuzi kunako ITV news eti walimu huko Tarime(Mara) wakiwa wamependeza kwenye matenge na malemba yao ya Ki-naijeria na original wax za Holland huku vidume vikiwa vimejaa na 'profile' zao na makoti ya suti ya mtumba, wameandamana benki. Kisa mshahara umechelewa kuingia. You know there are pipo who despise and insult HakiElimu kwamba ni wachochezi kumbe masikini hawa akina Rajesh know what they are saying and they've gone to the field for it. Sijui Mungai alijisikiaje aipoona ile hali!!! Walimu hawana kiu na mbado you are expecting much from them, really!! Be eyes.
Ipo hii nyingine; ni kuhusu hawa wa 'Crash-programme.' serikali haitasema lakini najua haikufanikiwa. Unaona bwana, karibu 1500 ninaestimate hawakuripoti. Mdogo wangu Imma ni mmoja wao; ktk shule aliyopangiwa huko Upareni ilitakiwa waende wa3 lakini wameripoti wa2, pale Ifati sec. wa3 karipoti m1 na rafiki yangu Rawlings pale Bomang'ombe karipoti peke yake kati ya wa3 waliopangwa. Government money spent well!!! kudos
Halafu bado ipo kali, umemchukua mtoto wa watu ndiyo kwanza katoka form six umemtrain for a month or so, unampeleka kunako shule wapi huko sijui na bado humlipi mshahara kwa more than 3 months eeh!
I gets me nuts!



No comments: