Dec 13, 2008

Wrist watch(s) story....

I got my first wrist watch nilipokuwa std. III au IV sikumbuki vizuri, ilikuwa ni DISCO makonyezo flani very maarufu sana wakati huo na hata siku hizi bado naziona mnadani pale Gorofani (alt spelling Gorfani), ya pili ilikuwa ni hizi za Kichina aka Hwang Hu, rangi ya gold kimtindo na ilikuwa grad present from dad I think, nikaigawa. Ya tatu nilinunua mwenyewe nilipojiunga na MWUCE ili kulua muda, nilikuwa nimetoka sec kule kuna kengele, lakini hapo kukawa hakuna, ikanibidi. Sasa huyu mama ambaye napiga mikonozzzz naye amenipatia saa yangu ya mkono(ni) ya NNE!!! Ana duka la vitabu hapa Cordoba "Libreria la Carmen". Good person, talkative like all Spaniards, well we couldn´t speak. She doesn´t speak English and I don´t speak Spanish, but it was bonitó.

My friends

Mama alitualika kwa msosi, dogo kule ni DJ.

Lola, Manuel na wengine, tulikuwa klub hapo.


Blanca and Ana

Dec 12, 2008

Mezquita





Hii ni landmark maarufu sana hapa Cordoba, in fact ni kama alama ya Cordoba, yaani huwezi kuzungumza kuhusu huu mji bila kutaja "Mezquita". Mwanzoni, historia na archeology zinadai ilikuwa ni "cathedral" ambalo baada ya uvamizi na conquest ya Wislamu (Waarabu?) walibalisha matumizi na kuwa msikiti maridhawa. Wakristo waliwashinda na kuwafukuza Waarabu (Moors) hao kama 1200 hivi na ku-regain jengo hilo ambalo mpaka sasa ni "catedral" ya dayosisi ya Cordoba.



Nahudhuria Jubilee

Hapa tupo La Mancha, katikati mwa Spain, tambarare sana hapa na kilimo kwa sana. Ni kijiji alichozaliwa Pd Miguel, El Toboso has about 2000 inhabitants, robust and beautiful.

Pd Miguel, the celebrant na Pd Pepe wakipiga miayo kabla ya msosi kuwasili.

Plate iko empty lakini ashaanza kula kichokoa meno, anajifanya Mhe. Temba nini? Mi amigo D. Paco

Wacha mambo yako watu tunagonga menyu.... Ni kama anasema vile, Pd Miguel Angel

Mdau nawakilisha Mang´ola

Sherehe...!


Cerveza (biere) zimekolea hapo ni kama glass ya 8 hivi, imnimwagikia kunako trousser, wananiambia ni alama kuwa sherehe iko pwa! Asikwambie mtu.
Hata sikumbuki nilimwambia nini vile...


Kama vile na-brush skills? Hamna kitu.....

Moshiiii! Mwanaume watu mitaa hii wanakula mafegi Mungu anajua!

Nilikuwepo kwa TV News jana

Click hapa kwenye link hii kuna kaji-video hapa afu forward hadi muda usome 18:50min-22:27min hapo ndipo kinachonihusu kinapoanza, tafsiri ya kilichosemwa (mi mwenyewe sijui kilichosemwa!) kwa sasa sina lakini naahidi kuitafuta. Now my pimpled face is all ova Spain.

Nakam Back

Kuna waliofikiri nitazamia, aah wapi! Ya huku nimeyaona na ninafikiri ni bora kula sahani moja na mafisadi wenzangu huko hom kuliko ku-stay mitaa hii. Kwa hiyo esta mañana nakwea pipa toka Madrid to Amsterdam afu baadae naunganisha mpaka KIA. Kwa hiyo tukutane holidei nyumbani, kama kawaida nakwenda kwa hija Kilema.