Apr 13, 2007

Ze Dustbin!

Ndugu wadau haka kaPasaka kanakoishia-ishia nilikuwa mgombani aka Moshi. Leo naandika kwa sababu kuna vitu viwili hivi nilivyoviona nataka ku-share.
Kwanza, usafi. Inawezekana na ninakubali kuwa Moshi ni kamji kadogo, pia hakana population kubwa hasa ikifika jioni kwani waChagga wote hukimbilia Machame, Marangu, Kiwoso, Mwika na kwingineko kulala lakini jamani Moshi kusafi. Kilichonivutia zaidi ni hawa akina mama wauza ndizi mbivu. Wako wengi siku hizi pale Moshi. Wanatembeza ndizi zao kichwani mji mzima. Wao tofauti na sehemu nyingine, ukinunua ndizi na ukaonyesha dalili kwamba utaila hapohapo, watakusubiri umenye, ule halafu wachukue ganda. Nilimuona mmoja kabeba ndizi kwenye sijui tenga lile? Pamoja na maganda yake. Halafu akafika kwenye “dustbin” (Kiswahili hapa nini?, kopo la taka?; kiwekea taka?; Msaada kwenye tuta!) nakumbuka ilikuwa ni pale Kibo Coffee Bar, akasimama aka-unload maganda aliyokusanya kwenye mizunguko yake akaondoka. Umombo hapa ; I was really moved!

Pili, vitambulisho kwa chingaz pale bus stand. Kumbe hili nalo linawezekana, kuwawezesha vijana wajasiriamali kutambulika kama waajiriwa wengine. Pale kituo kikuu cha mabasi wana kautaratibu ambako kamenifurahisha. All chingaz aka wamachinga aka marching guys/ladies wana vitambulisho na sare? (uniform). Wauza mkate, wauza matunda wote, moja wanavaa makoti (kama yale ya waganga) meupe au hudhurungi mgongoni ymeandikwa kwa maandishi makubwa:

  • Muuza mikate Stend: Fuata sheria za Stendi
  • Muuza matunda (ndizi?): Fuata sheria za Stendi
  • Chinga Room No. XX: Fuata sheria za Stendi

Mbili wana vitambulisho vyenye picha, jina na stamp ya meneja wa stand. Safi hiyo!
Mimi nafikiri hii ni changamoto kwa town councils, municipalities na city councils nyingine hapa TZ na East Africa kwa ujumla na pia kwetu cityzens kwamba usafi unaanza na sisi wenyewe. Halafu baadae waje site (soma ilivyo sio neno la kiIngereza) au manispaa.
Kalaghabaho!!!

No comments: