Dec 1, 2009
Siku ya UKIMWI Mang'ola
Leo ndo the World AIDS day, na huku Mang'ola tumeidhimisha kwa marefu na mapana yake. Huku kuna NGO inaitwa Msamaria Mwema, imeanzishwa na mapadri wa misheni ya Mang'ola Chini. Hawa watu wamefanya maandamano, ngoma, ngonjera, mashairi na hotuba kama ilivyo ada katika siku hii. Lengo ni kupeleka ujumbe 'UKIMWI upo, unaua, hauna tiba, unaweza kuzua maambukizi kuendelea kama utatimiza wajibu wako'
Mang'ola inawakilisha almost kila kabila ya nji hii na nchi jirani pia. Wengi huku ni wa-kuja. Kitunguu bwana! Population ya hapa ina-represent almost 19% of people of Karatu district as of 2002 census. Now, huu mchanganyiko wa watu, kuwepo kwa hela 'nyingi' zitokanazo na kilimo cha vitunguu, na potful of other factors, maambukizi ya UKIMWI yako juu.
Kwa habari za juujuu eti viongozi wa serikali ya kijiji, kata n.k hawakuhudhuria. Inaonekana kwao hili janga si prayoriti; wengine wamesafiri, au wamekwenda shamba. Sawa lakini UKIMWI si ni sera ya govt? Luckily wamepatikan wanafunzi wa primary na secondary school kama 1000 hivi. Nikafurahi, kama tunaweza kuwaandaa hawa taifa la keshao, wakue wakiujua UKIMWI na yote yaliyomo; tutawahitaji viongozi wa serekali wa kazi gani? Nafikiri hii ni changamoto!!
Huduma kwa waathirika wa UKIMWI/VVU na upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusu gonjwa hili ni haki ya kila mmoja. Umekwishafanya nini?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment