Ndugu Mgeni Rasmi,
Mustakabali wa taifa letu na raia wake upo katika hatihati iwapo hali iliyopo sasa miongoni mwa viongozi wetu tuliowapa dhamana kubwa ya kuliongoza taifa hili hawatadhibitiwa. Ubinafsi uliokithiri, rushwa, ufisad, ubadhirifu wa mali ya umma, uhujumu uchumi, ujambazi, dhuluma, utapeli, mauaji ya imani za kishirikina, na uovu wa kila aina umekuwa ndio sera yao. Dhamira njema ya ukmbozi wa wananchi kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania itakuwa ndoto za alinacha kama hautakuwepo utashi wa dhati wa kisiasa wa kupanmbana na hali hiyo.
Jambo la kusikitisha ni kuendelea kukua kwa kasi kwa pengo llilopo baina ya wenye nacho na wasio nacho; yaani matajiri na maskini katika jamii ianyoamini katika misingi ya usawa wa binadamu. Katika jamii hii ya tabaka la wakulima na wafanyakazi; wapo watu wenye fedha nyingi na wanaishi maisha ya kifahari sana na kuwaacha wengine wengi ambao hata kupata mlo kamili wa siku ni shida. Wengi hawana ajira za kuamininka wala mitaji au elim ya ujasiriamali, wanajaribu kukopa mikopo midogo midogo wafanye biashara ili kujikwamua kiuchumi, lakini wapi! Wanazidi kutumbukia kwenye lindi la umasikini uliokithiri. Maisha yanakuwa ya samak baharini. Mkubwa kumla mdogo!
Vita dhidi ya maadui wakubwa wa jamii yetu; ujinga, umasikini, na maradhi imekuwa nadharia tu. Vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano vimeongezeka. Kipato cha Mtanzania kinazidi kushuka na thamani ya fedha yetu hali kadhalika. Utandawazi ulikusudiwa kutupatia wajomba kwa jina maarufu “wawekezaji” ili waje kutukwamua kiuchumi.wote tuliweka matumaini ya kukua kwa uchumi, kuongezeka kwa nafasi za ajira katika viwanda, migodi, mashamba, mabenki, mashirika namakampuni katika sekta binafsi. Hata hivyo hali si ya kuridhisha, “wajomba” wengi wanatula “usogo”. Wanakula vyetu huku wanatung’ong’a.
Wanawasainisha waheshimiwa wetu mikataba ya ulaghai na wanatumia udhaifu uliomo ndani ya mikataba hiyo kuhamisha utajiri wetu kwenda kwao. Madini, mabo hata wanyama! Maskini, wajinga ndio waliwao. Usimwamshe aliyelala usije ukalala wewe!
Leo hii kumeanza kuzuka migogoro ya kugombea ardhi baina ya wakulima na wafugaji, wawekezaji na wanakijiji, viongozi na raia. Hali hii si dalili nzuri kwa taifa letu, amani tunayojivunia kwa kitambo sasa tunaiweka rehani. Ukiona vyaelea vimeundwa!
Hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha. Dalili ya mvua ni mawingu. Dalili za Watanzania kuzinduka kutoka kwenye usingizi mzito zimeanza kuonekana. Tunaanza kufuta tongotongo. Hoja za kuhoji na hatimaye mikakati ya kurejea baadhi ya mikataba tuliyoingia kichwa kichwa zinaonesha kla dalili za kiwingu cha mageuzi na ni hatua ya kujivunia. Mapambani dhidi ya ufisadi na uimarishaji wa demokrasia na miundombinu ya nchi ni hatua ya mafanikio. Wabunge bila shaka mtaendelea kuisaidia serikali na sekta binafsi kuboresha mazingira yaliypo ili kusaidia kuinua uchumi wa nchi yetu na wa mtu mmoja mmoja. Changamoto kubwa mliyo nayo ni kubuni nafasi za ajira na kuongeza mitaji kwa makundi yote ya kijamii.